Rais wa China Xi Jinping amekutana na ofisa mkuu wa Mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong Bi. Carrie Lam Cheng Yuet-ngor, na ofisa mkuu wa Mkoa wa utawala maalumu wa Macao Bw. Fernando Chui Sai On, na kupata maelezo juu ya hali ya sasa ya Hong Kong na Macao na kazi ya serikali ya mikoa ya utawala maalum. Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa ili kukabiliana siku zijazo, inatakiwa kushikilia kanuni ya "Nchi Moja na Mifumo Miwili" na kusaidia Hong Kong na Macao katika kuunganishwa katika hali ya jumla ya maendeleo ya kitaifa, kutimiza maendeleo mapya, na kutoa michango mpya.
Rais Xi Jinping amesema kuwa katika miaka 40 iliyopita tangu sera ya mageuzi na ufunguzi wa mlango itekelezwe, wakazi wa Hong Kong na Macao ni mashahidi na washirika, vilevile ni wanaonufaika na wachangiaji. Wakazi wa Hong Kong na Macao ni kama walivyo wakazi wa Bara la China, wote ni wavumbuzi wa miujiza mikubwa iliyopatikana katika mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |