• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gazeti la Renminribao latoa tahariri ya kuadhimisha miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango

    (GMT+08:00) 2018-12-18 10:02:54

    Gazeti la Renminribao la China leo limetoa tahariri yenye kichwa cha "mwujiza mkubwa zaidi katika zama mpya, miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango".

    Tahariri hiyo imesema, mwaka 1978, China ilianzisha mchakato wa mageuzi na kufungua mlango katika mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 11 ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kuibadilisha China kwa kina, na kuwa na ushawishi mkubwa duniani.

    Tahariri imesema, katika miaka 40 iliyopita, tangu Majadiliano kuhusu Vigezo vya Ukweli yafanyike, mageuzi na kufungua mlango siku zote ni wito wa kizama kote nchini China. Hivi leo chama tawala cha China kinataka kueleza "nchi ya kijamaa ya China inaelekea wapi", na kimefanikiwa kuanzisha njia maalumu ya China ya kutimiza mambo ya kisasa, nchi ambayo ilikuwa kwenye "hatari ya kutengwa na dunia" imekuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani, na imejitahidi kutimiza ustawi tena kutoka karne iliyopita, na kufanikiwa kuwa "kiongozi wa zama" kutoka "mfuasi wa zama".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako