• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuielewa China kutoka pande tatu, Mwaka huu ni madhimisho ya miaka 40 ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi ya China, jumuiya ya magharibi imetoa maswali mengi kuhusu "China itaelekea wapi katika siku za baadaye?"

  (GMT+08:00) 2018-12-18 10:37:15

  Mwaka huu ni madhimisho ya miaka 40 ya utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi ya China, jumuiya ya magharibi imetoa maswali mengi kuhusu "China itaelekea wapi katika siku za baadaye?", "China ni mwenzi au mshindani?","China ni fursa au changamoto?" Kwa kukabiliana na hali hiyo, mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu "Kuielewa China" umefanyika hapa Beijing.

  Mkutano huo umewavutia watu karibu 600 wakiwemo wanasiasa, wanamkakati na wafanyabiashara 40 maarufu duniani. Rais Xi Jinping wa China pia ametoa pongezi kwa mkutano huo huku akisisitiza kuwa China itaendelea kuimarisha mageuzi na kuzidi kufungua mlango wazi, kushikilia utekelezaji wa wazo la maendeleo mapya, kuhimiza uchumi wa China kuendelezwa kwa kiwango cha juu na kutoa fursa nyingi zaidi za ushirikiano kwa dunia.

  Jumuiya ya kimataifa hasa nchi za magharibi ina mijadala mingi kuhusu China ambayo inaweza kujumuishwa kwa maswali matatu yaani "China ni nchi ya aina gani?","China inatoka wapi?" "China itaenda wapi?".

  Kuhusu swali la kwanza, mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Yang Jiechi ametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo ikisema, jumuiya ya kimataifa inaweza kuielewa China kutoka pande mbalimbali ambazo ni pamoja na China inashikilia maendeleo ya amani, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana, kushikilia usawa na haki, kupendekeza usalama wa pamoja.

  Kwa swali la pili, mkuu wa kamati ya utafiti wa mkakati wa uvumbuzi na maendeleo ya taifa ya China Bw. Zheng Bijian ametumia "pande mbili " kueleza maendeleo na upungufu wa China. Kwa mfano, kwa upande mmoja, China ni nchi kubwa ya utengenezaji wa bidhaa duniani, kwa upande mwingine uwezo wa utengenezaji wa bidhaa bado uko katika kiwango cha chini.

  Swali la tatu ni kwamba China itaenda wapi? Washiriki wa mkutano huo wanaona kuwa jibu la swali hilo ni wazi na dhahiri, yaani lengo la maendeleo ya uchumi na jamii lililotolewa na mkutano mkuu wa 19 wa wajumbe wa chama cha CPC ambalo ni pamoja na kujenga kwa pande zote jamii yenye maisha bora hadi mwaka 2020, kutimiza ujamaa wa kisasa hadi mwaka 2035 na kujenga nchi ya ujamaa wa kisasa yenye ustaarabu, utajiri, demokrasia, masikilizano na uzuri hadi katikati ya karne hiyo.

  Maoni hayo yalikubaliwa na waziri mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown. Alipotoa hutuba alisema, wazo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja litathibitishwa na hali halisi, pia litathibitishwa mapema kuliko watu walivyotarajia. Vilevile alitoa wito wa kujenga dunia inayofungamana, alisema hivi sasa binadamuu wanahitaji kupinga sera ya kujilinda kwa kupitia ushirikiano wa kimataifa.

  Wakati wa kuadhimisha miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, wanasiasa, wanamkakati na wanakampuni duniani walikusanyika hapa Beijing, ambapo watachambua nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo ya China kwa pande za mkakati wa maendeleo ya kikanda, uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, uboreshaji wa viwanda na ujenzi wa mfumo wa fedha wa kisasa, pia watatafuta fursa mpya za ushirikiano wa kimataifa kwa pande za usalama wa kikanda, uhusiano mpya wa kimataifa na ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Hii si kama tu itazifanya nchi za Magharibi ziielewe China vizuri zaidi, bali pia itainufaisha dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako