• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaadhimisha miaka 40 ya sera ya mageuzi ya ufunguaji mlango

    (GMT+08:00) 2018-12-18 10:41:53

    China imefanya sherehe kubwa ya maadhimisho ya miaka 40 tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, ambayo ni mapinduzi makubwa ambayo yamebadilisha mwelekeo wa China na kuleta ushawishi duniani.

    Sherehe ya maadhimisho hayo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya umma mjini Beijing na kuhudhuriwa na Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang aliongoza sherehe hiyo ya maadhimisho. Mjumbe wa kamati ya kudumu ya kamati ya siasa ya chama cha kikomunisti cha China Bw. Wang Huning alisoma orodha ya majina ya watu waliotoa mchango mkubwa kwenye utekelezaji wa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako