Mkutano wa maadhimisho ya miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango umefanyika leo mjini Beijing. Rais Xi Jinping ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na mwenyekiti wa Baraza la kijeshi la kamati hiyo amehudhuria na kuhutubia mkutano huo.
Katika miaka 40 iliyopita, nguvu ya China imeongezeka kwa kiasi kikubwa, wastani wa kasi ya ongezeko la uchumi kwa mwaka ni asilimia 9.5, wastani wa pato la wananchi umeongezeka mara 22.8, idadi ya watu maskini imepungua kwa watu milioni 740, na thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje imeongezeka kwa mara 198. Hadi sasa China imekuwa nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi, na nchi ya kwanza katika sekta za viwanda na biashara ya bidhaa, na nchi ya kwanza yenye kiasi kikubwa cha akiba za fedha za kigeni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |