Rais Xi amesisitiza kuwa uvumbuzi ni uhai wa sera ya mageuzi na kufungua mlango. Amesema kwenye njia ya maendeleo ya China, inapaswa kushikilia Umax-Lenin, Fikra ya Mao Zedong, Nadharia ya Deng Xiaoping, uwakilishi wa matakwa ya maendeleo ya nguvukazi ya kisasa ya China, mwelekeo wa kusonga mbele wa utamaduni wa kisasa wa China na maslahi ya kimsingi ya wananchi walio wengi kabisa wa China, wazo kuhusu kujipatia maendeleo kwa njia ya kisayansi, na ujamaa wenye umaalumu wa China wa zama mpya, kushikilia kuunganisha kihalisi ukombozi wa kifikra na kutafuta ukweli kutokana na hali halisi. Pia ni jukumu la wanachama wa Chama cha kikomunisti cha China kuendeleza U-marx wa karne 21, na u-marx wenye umaalum wa China ya kisasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |