Rais Xi Jinping wa China amesema China inapaswa kuendelea kufuata njia ya kuendeleza ujamaa wenye umaalum wa China ambayo inafaa zaidi China kuongoza maendeleo ya zama hii. Amesema katika sera ya mageuzi na kufungua mlango ya China, China inapaswa kugeuza njia za kufuata maslahi ya maendeleo ya mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa China, kusukuma mbele mfumo wa utawala wa nchi na uwezo wa kisasa wa utawala. China pia inapaswa kutambua kwa wazi jambo linalopaswa kubadilishwa na lisiloweza kubadilishwa. Pia amesisitiza kuwa, China inapaswa kushikilia kuendeleza uchumi kuwa kazi ya msingi, kushikilia kanuni nne za msingi na kuendelea kutekeleza mageuzi na kufungua mlango.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |