Rais Xi Jinping wa China amesema, China inapaswa kuendelea kuboresha mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa China, na kuendelea kukuza na kuongeza ubora wa mfumo huo. Amesema, China inatakiwa isibadilishe kamwe kuimarisha na kuendeleza uchumi unaomilikiwa na dola, kuunga mkono na kuhimiza maendeleo ya uchumi binafsi. Pia inapaswa kujitahidi kuondoa vizuizi vyovyote vya mfumo wa maendeleo na usawa katika jamii, kuharakisha kujenga mfumo kamili wenye kanuni za kisayansi na ufanisi mkubwa, na kuimarisha mfumo wa ujamaa wenye umaalum wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |