• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Asante Kotoko ya Ghana yatia aibu kwa kuiba taulo za hoteli Kenya

    (GMT+08:00) 2018-12-19 09:14:26

    Ilikuwa aibu ya mwaka kwa kikosi cha Asante Kotoko kumulikwa kwa kuiba taulo za uso katika hoteli moja jijini Nairobi baada ya mechi yao ya kuwania ubingwa wa Kombe la Mashirikisho (CAF) dhidi ya Kariobangi Sharks Jumamosi Disemba 15 kwenye uga wa MISC Kasarani. Wachezaji wa timu hiyo kutoka Ghana wanadaiwa kutoka hotelini humo na taulo hizo kati ya bidhaa nyingine, tukio ambalo Afisa Mkuu Mtendaji wa klabu George Amoako ametaja kuwa halikupaswa kutokea. Sare tasa iliyosajiliwa Jumamosi na timu hizo mbili inaiweka Asante Kotoko katika hatua nzuri ya kufuzu iwapo itaifunga Kariobangi Sharks na pia kujiepusha na sare ya idadi yoyote ya mabao. Mechi ya marudiano itagaragazwa katika uwanja Baba Yaro Sports Stadium mjini Kumasi Disemba 22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako