• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Serengeti Boys kushiriki mashindano maalumu ya maandalizi ya Afcon U17

    (GMT+08:00) 2018-12-19 09:14:41

    Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania U17 "Serengeti Boys" itashiriki mashindano maalumu ya maandalizi ya Afcon chini ya miaka 17 yatakayofanyika Antalya nchini Uturuki mapema mwakani. Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania TFF kupitia tovuti yake. mashindano hayo yameandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA, ambapo yanatarajia kuanza Februari 22,2019 mpaka Machi 2,2019 na kushirikisha jumla ya timu 12 kutoka Afrika na Ulaya. Mbali na Serengeti Boys, nchi nyingine za Afrika zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Angola, Morocco, Cameroon, Uganda, Nigeria, Senegal na Guinea ambazo zitaungana na timu nne kutoka bara la Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako