• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Kibarua cha Jose Mourinho chaota mbawa, Pogba roho kwatu

  (GMT+08:00) 2018-12-19 09:37:33

  Kocha Jose Mourinho ameondelewa katika nafasi yake ya kuinoa klabu ya Manchester United baada ya kuiona klabu hiyo kwa miaka miwili na nusu. Aliyewahi kuwa nahodha wa klabu hiyo, Michael Carrick anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo hadi mwisho wa msimu. Hata hivyo muda mchache baada ya Mourinho kutimuliwa mchezaji ghali zaidi ndani ya timu hiyo Paul Pogba ameonesha kufurahishwa na uamzi huo. Kupitia mtandao wa Twitter Pogba ameweka picha iliyoambatana na ujumbe unaotaka wafuasi wake kuweka maoni yao juu ya picha hiyo. Lakini Pogba aliifuta picha hiyo baada ya muda mfupi. Naye mkongwe wa klabu hiyo ambaye pia ni kocha, Gary Neville ameunga mkono ujumbe wa Pogba kwa kuuandika na kuweka kwenye ukurasa wake. Vyanzo mbalimbali vinataja makocha kadhaa wanaoweza kuchukua nafasi ya Mourinho mwisho wa msimu huu baada ya klabu kuweka wazi kuwa kocha wa muda atakayetangazwa ndani ya saa 48 atadumu hadi mwisho wa msimu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako