• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kushuhudia, kushiriki, kuchangia na kunufaishwa kwa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi ya China

    (GMT+08:00) 2018-12-19 20:54:19

    Sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi ya China iliyozinduliwa mwaka 1978 ilibadilisha China na pia kuathiri dunia. China ikiwa nchi inayofahamu kushukuru, wakati inapokumbusha mafanikio yaliyopatikana katika miaka 40 iliyopita, haiwezi kusahau wageni waliowahi kutoa msaada na uungaji mkono kwa China.

    Katika mkutano wa kuadhimisha miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango wazi, rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu akitoa shukrani kwa marafiki wa kigeni na watu wa nchi mbalimbali duniani wanaofuatilia na kuunga mkono mageuzi na ufunguaji mlango wazi wa China. Wakati huohuo, wageni kumi wamepata "tuzo ya urafiki uliopatikana katika mchakato wa mageuzi ya China", ambao ni pamoja na Alain Mérieux aliyeisaidia China kukabiliana na mgogoro mkubwa wa afya ya umma wa SARS na homa ya mafua ya ndege, Werner Gerich aliyekuwa mkuu wa kigeni wa kwanza aliyeajiriwa na kiwanda cha taifa nchini China, Klaus Schwab aliyeisaidia China kujiunga na uchumi wa dunia, Konosuke Matsushita aliyesaidia maendeleo ya viwanda vya kielektroniki vya China, Lee Kuan Yew aliyeunga mkono kithabiti "Mtindo wa maendeleo wa China" na Juan Antonio Samaranch aliyeisaidia China kurudi katika familia ya michezo ya Olimpiki. Waliopewa tuzo hizo wanatoka kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, utengenezaji wa bidhaa, teknolojia ya kielektroniki, michezo, huduma na uchumi na fedha, lakini wote walishuhudia na kuchangia mageuzi na ufunguaji mlango wazi wa China.

    Hali halisi ni kwamba, maelfu ya wageni wameshiriki na kutoa mchango katika mageuzi na ufunguaji mlango wa China. Washindi wa tuzo hiyo si kama tu wamekuwa alama ya China inayofungua kwa dunia, bali pia wamehimiza kazi, shughuli na miradi katika mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango. Marafiki wengi wa kigeni wametoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa sera hiyo, ambao hawatasahauliwa na wachina.

    China imepata maendeleo makubwa, huku ikinufaisha dunia. Soko kubwa la China limekuwa msukumo mpya wa uchumi la makampuni mengi ya kimataifa. Katika miaka mingi iliyopita, China imechangia zaidi ya asilimia 30 ya uchumi wa dunia. Tokea mwaka 2013 hadi 2017, China imetoa nafasi zaidi ya laki 2 za ajira katika maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi uliojengwa nao na nchi za "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Tangu mwaka 2004, China imetoa misaada zaidi ya mia 3 ya kibinadamu ya kimataifa, ambayo inaongezeka kwa asilimia 29.4 kila mwaka. Mbali na kushiriki katika operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, China pia imesamehe madeni ya nchi zilizoko nyuma kimaendeleo, kutoa dola zaidi ya bilioni 60 za kimarekani kwa nchi za Afrika. Kama rais Xi Jinping alivyosema katika hotuba yake, China inazidi kuelekea katikati ya jukwaa la dunia, na kuwa mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia, mlinzi wa utaratibu wa kimataifa anayetambuliwa na jumiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako