• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Gunnar Solskjaer katangazwa kuchukua mikoba ya Jose Mourinho Man United

  (GMT+08:00) 2018-12-20 08:39:53

  Klabu ya Man United jana imlifikia maamuzi ya kumtangaza kocha wao mpya wa muda atakayerithi mikoba ya kocha Jose Mourinho katika club hiyo, uamuzi huo umetangazwa ikiwa ni siku moja tu imepita toka Man United itangaze kusitisha ajira ya Jose Mourinho ndani ya Old Trafford. Man United imemtangaza mchezaji wao wa zamani raia wa Norway, Ole Gunnar Solskjaer kuwa ndio kocha wao mpya hadi mwisho wa msimu wa 2018/2019 watakapotangaza kocha mpya wa kudumu. Ole Gunnar Solskjaer atakuwa kocha wa Man United akishirikiana na Mike Phelan na Michael Carrick na Kieran McKenna. Kama utakumbuka Ole Gunnar Solskjaer aliwahi kuwa mchezaji wa Man United kuanzia mwaka 1995 hadi 2007 na aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Norway. Kabla ya kujiunga na Man United kama kocha wa muda Solskjaer alikuwa akiifundisha Molde na amewahi kuifundisha Cardiff City na timu ya Man United ya wachezaji wa akiba.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako