• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raga: Raga Afrika yaitangaza Kenya kuwa mwandaaji wa Michuano ya Raga Barthes ya Afrika U-20

    (GMT+08:00) 2018-12-20 08:41:14

    Shirikisho la Raga Afrika limethibitisha kuwa Kenya itakuwa mwandaaji wa Michuano ya Raga Barthes ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 mwezi Machi mwakani mjini Nairobi. Mashindano hayo yatashirikisha timu za taifa chini ya miaka 20 kutoka Namibia, Chipu ya Kenya, Senegal na Tunisia. Zimbabwe na Madagascar zimetolewa kwenye Pool A na kuingia divisheni ya pili na nafasi zao kuchukuliwa na Senegal na Tunisia baada ya kampeni ya mwaka 2018. Mshindi wa Pool A atafuzu kucheza kombe la dunia la Raga mwaka 2019 lililopangwa kufanyika Estádio Martins Pereira huko São José dos Campos, Brazil kuanzia Julai 9 hadi Julai 21. Zimbabwe itaandaa michuano ya divisheni ya pili ya Afrika ya vijana chini ya miaka 20, ambayo pia inajulikana kama Pool B, Aprili mwakani. Morocco, Madagascar na Ivory Coast zitashiriki michuano hiyo itakayokuwa ya wiki nzima ambapo mshindi atapandishwa na kuingia Pool A.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako