• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Gareth Bale afukuzia kiatu cha dhahabu katika mashindano ya Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia

  (GMT+08:00) 2018-12-21 09:57:25

  Mshambualiaji Gareth Bale wa Real Madrid, ameonyesha nia ya kutaka kuondoka na kiatu cha dhahabu katika mashindano ya Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia. Mshambuliaji huyo juzi alifunga mabao matatu 'hat-trick' na kuiwezesha timu yake kuizamisha Kashima Antlers ya Japan kwa mabao 3-1 katika mechi ya nusu fainali na sasa itacheza fainali na wenyeji Al Ain ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Kocha wa Real, Santiago Solari, alimfagilia Bale, ambaye amefikisha mabao sita katika mechi tano walizocheza hadi sasa, huku Real ikiwania kutwaa taji la tatu mfululizo la michuano hiyo. Mechi ya fainali itachezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Zayed Sports City, mchezo unaoonekana kuvuta hisia za wengi ikizingatiwa Al Ain ya Abu Dhabi iliwaduwaza wengi baada ya kuing'oa kwa penalti bingwa wa Amerika ya Kusini, River Plate ya Argentina.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako