• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yasema kuwa ujumbe wa China na Marekani umejadiliana kuhusu mipango ya kipindi kijacho

    (GMT+08:00) 2018-12-21 16:38:55
    Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, ujumbe wa China na Marekani unadumisha mawasiliano ya karibu, na umefanya majadiliano halisi kuhusu mipango ya kipindi kijacho. Bw. Gao Feng amesema, lengo la majadiliano kati ya China na Marekani ni kutatua ipasavyo migogoro ya kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili. Iwapo zitazingatia ufuatiliaji wao wa pamoja, hakika zitaweza kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

    Mwanzoni mwa mwaka huu, viongozi wa China na Marekani walifanya mazungumzo huko Buenos Aires, Argentina, wakikubaliana kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili unaofuata msingi wenye uwiano, ushirikiano na utulivu, na kufikia makubaliano kuhusu suala la kiuchumi na kibiashara, na kusimamisha kutozana ushuru mpya wa forodha. Msemaji wa Wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng anasema:

    "Tangu viongozi wa China na Marekani walipokutana, ujumbe wa pande hizo mbili umedumisha mawasiliano ya karibu, na kufanya majadiliano halisi kuhusu mipango ya kipindi kijacho. Pande hizo mbili zitapanga shughuli mbalimbali zikiwemo mazungumzo ya ana kwa ana, na kwa njia ya simu kwa kufuata maendeleo ya majadiliano, ili kuhimiza utekelezaji wa maafikiano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa pande hizo mbli."

    Jambo linalofuatiliwa na watu ni kwamba, tangu viongozi wa nchi hizo mbili walipokutana kwenye Mkutano wa kilele wa G20 na kufikia maafikiano, Kamati ya utungaji wa kanuni kuhusu ushuru wa forodha kwenye Baraza la Serikali la China imeamua kusimamisha utozaji wa ushuru kwa miezi mitatu kwa magari na vipuri vyake vinavyotengenezwa nchini Marekani kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Machi mwaka ujao. Wakati huo huo Ofisi ya wajumbe wa biashara ya Marekani pia imeahirisha muda wa kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 200 za China hadi tarehe 2 Machi mwaka 2019. Bw. Gao Feng anaona kuwa hatua hizo za pande hizo mbili zimeonesha ishara chanya kwa mwelekeo wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, kwani lengo la majadiliano kati ya pande hizo mbili ni kutatua ipasavyo migogoro ya kiuchumi na kibiashara. Mwaka huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 40 tangu kutolewa kwa taarifa ya pamoja kuhusu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani. Bw. Gao Feng anasema:

    "Upande wa China unaona China na Marekani zikiwa nchi kubwa zina maslahi makubwa zaidi ya pamoja kuliko mikwaruzano iliyopo kati yao katika sekta ya uchumi na biashara. Umuhimu wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara katika uhusiano kati ya pande hizo mbili hautabadilika, na kiini cha kunufaishana katika uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili pia hakitabadilika. Tokea mwaka huu, licha ya mikwaruzano ya kibiashara, mahitaji na mustakabali wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili bado ni mpana sana. Watu wengi wametambua kuwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili unapaswa kurudi kwenye njia ya kawaida."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako