• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya uwekezaji wa miundo mbinu ya Asia na Benki ya maendeleo mapya ya BRICS zapewa hadhi za waangalizi wa baraza kuu la UN

    (GMT+08:00) 2018-12-21 17:20:32

    Baraza kuu la 73 la Umoja wa Mataifa jana limepitisha maazimio na kuzikaribisha Benki ya uwekezaji wa miundo mbinu ya Asia na Benki ya maendeleo mapya ya BRICS kushiriki kwenye mkutano na shughuli za baraza kuu la Umoja huo zikiwa waangalizi wake.

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, kupewa hadhi za waangalizi wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kwa benki hizo mbili, kuna umuhimu mkubwa kwa kuhimiza zaidi majukumu ya maendeleo endelevu duniani.

    Balozi Ma amesema, ikiwa nchi mwenyeji wa benki hizo mbili, China ilitoa miswada ya maazimio hayo mawili, ambayo yamekaribishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Amezitaka benki hizo mbili zioneshe umuhimu zaidi kwenye maendeleo ya kimataifa, na kuhimiza zaidi ushirikiano wa maendeleo duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako