• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sheria ya Marekani kuhusu Xizang yaingilia kati mambo ya ndani ya China

    (GMT+08:00) 2018-12-22 17:13:02

    Ikulu ya Marekani hivi karibuni ilipitisha Sheria kuhusu masuala ya wageni Kuingia Xizang, Mwaka 2018 iliyopitishwa na bunge la Marekani, na hivi sasa sheria hiyo imekuwa rasmi nchini humo. Sheria hiyo pia inaitwa Sheria ya Kusafiri kwa Usawa, kwa mujibu wa sheria hiyo, serikali ya China inalazimika kuwaruhusu waandishi wa habari, wanadiplomasia na watalii kutoka Marekani kuingia Xizang bila vizuizi vyovyote, ama sivyo maofisa hao waliotunga sera na kuwazuia wamarekani kuingia Xizang watazuiliwa kuingia nchini Marekani. Sheria hiyo inaonekana kuwa inajaribu kuwapa haki wamarekani kuingia Xizang kwa uhuru, lakini kihalisi inaonesha wazo la Kipaumbele cha Marekani, na wazo la kuweka sheria ya ndani ya Marekani juu ya sheria ya kimataifa.

    Xizang ni sehemu isiyotengwa na China siku zote. Kitendo cha Marekani si kama tu kimekiuka kanuni za kimsingi za mawasiliano kati ya nchi kwenye uhusiano wa kimataifa, bali pia kimeingilia kati mambo ya ndani ya China.

    Siku zote China haiwazuii wageni wanaopenda kuingia China wakiwemo wamarekani kutalii Xizang. Baadhi ya wabunge wa Marekani pia walifanya ziara huko Xizang, na wamarekani wengi walikwenda Xizang mara nyingi.

    China si kama tu haiwazuii wageni kwenda Xizang, bali pia inafanya juhudi kutangaza historia, utamaduni, na mabadiliko ya sasa ya Xizang kwa nje, ili kuwavutia watu wengi kuzingatia Xizang, serikali ya huko ilichukua hatua mfululizo. Xizang iliyofungua milango nchini China inawakaribisha watu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako