• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Simba ya Tanzania yalipiza kisasi dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-24 09:02:49

    Simba SC jana ilivunja rekodi yake mbaya dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba walikuwa nyumbani uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa marudiano round ya kwanza. Katika mchezo huu Simba SC walikuwa wakihitaji ushindi wa kuanzia goli 1-0, hiyo ni baada ya mchezo wa kwanza walioucheza Kitwe Zambia, kufungwa kwa magoli 2-1, presha ilikuwa kubwa katika mchezo huo ikizingatiwa Simba hawakuwahi kuwatoa Nkana mara zote walizocheza. Simba licha ya kutanguliwa kwa goli la mapema na kupewa mzigo wa kuhitaji magoli matatu ili wafuzu, walifanikiwa kupindua matokeo na kuwafunga Nkanda Red Devils kwa magoli 3-1 na kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 10 toka washiriki kwa mara ya mwisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako