• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baiskeli: Mrwanda Joseph Areruya awa Mwendesha baiskeli wa Mwaka 2018 wa Afrika

  (GMT+08:00) 2018-12-24 09:04:20

  Mrwanda Joseph Areruya, anayeendesha baiskeli katika timu ya Ufaransa Delko Marseille, Ijumaa alitajwa kuwa Mwendesha baiskeli wa Mwaka 2018 wa Afrika na kuwa Mrwanda wa kwanza kushinda tuzo ya juu tangu ianzishwe mwaka 2012. Mchezaji huyo mwenye miaka 22 mwaka jana alishindwa na Muafrika Kusini Louis Meintjes na kumaliza akiwa wa pili. Katika mashindano ya mwaka huu Areruya alifuatiwa na Muafrika Kusini Daryl Impey na Mueritrea Amanuel Ghebreigzabhier wakichukua nafasi ya pili na tatu mtawalia. Ushindi wake katika mashindano ya La Tropicale ya Gabon na Tour de l'Espoir ya Cameroun pamoja na medali zake nne katika mashindano ya Mabingwa wa Bara la Afrika mwaka huu umemfanya achukue tuzo hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako