• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa China kukua kwa utulivu

    (GMT+08:00) 2018-12-24 16:53:06

    Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ilifanya mkutano kuhusu kazi ya uchumi wiki iliyopita, ili kufanya majumuisho ya kazi ya uchumi kwa mwaka huu, na kupanga kazi ya mwakani.

    Huu si mwaka wa kawaida kwa uchumi wa China. Wakati mawazo ya kupinga utandawazi, mivutano ya kibiashara na hali ya kutatanisha ya uchumi wa dunia zinapoongezeka, jumuiya ya kimataifa inafuatilia jinsi China inavyohimiza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Mkutano wa kazi ya uchumi wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China umedhihirisha kuwa, China imedumisha maendeleo mazuri ya mfululizo ya uchumi na utulivu wa jamii, na kupiga hatua mpya katika kutimiza lengo la kujenga jamii yenye maisha bora.

    Kutokana na ongezeko la mivutano ya biashara kati ya China na Marekani, baadhi ya watu wana mashaka kuwa, fursa ya maendeleo ya uchumi wa China imefika ukomo. Mkutano huo umetoa jibu la hapana. Umesisitiza kuwa fursa hiyo bado itaendelea kuwepo kwa muda mrefu, licha ya kuwa China inakabiliwa na changamoto nyingi, mchakato wa utandawazi hautarudi nyuma, na nchi mbalimbali haziwezi kutengana kutokana na kuwa na ushirikiano karibu wa kiuchumi. Aidha, China ina soko kubwa, na kutoa mchango muhimu katika shughuli nyingi za kimataifa ikiwemo kupunguza umaskini, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kulinda amani.

    Mwaka 2019 ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, pia ni mwaka muhimu wa kutimiza lengo la kujenga jamii yenye maisha bora. Mkutano huo umedhihirisha kuwa, tatizo kuu la uchumi wa China ni muundo wa uzalishaji, hivyo China itaharakisha kupunguza uwezo wa uzalishaji wa kupita kiasi na gharama mbalimbali za uendeshaji, kukamilisha miundombinu, na kujenga mfumo wa kisasa wa soko. Mkutano huo pia umeagiza kukinga na kuondoa hatari kubwa, kupunguza umaskini, kushughulikia vizuri uchafuzi wa mazingira na kufanya vizuri kazi nyingine muhimu za kuhimiza maendeleo ya uchumi. Ili kutimiza malengo hayo, mkutano huo umetoa hatua nyingi muhimu, ikiwemo kuunda upya mfumo wa maabara muhimu ili kuongeza uwezo wa uvumbuzi wa uzalishaji, kupunguza kodi ili kuongeza uwezo wa kujiendeleza wa kampuni na uwezo wa ununuzi wa wananchi, na kulinda maslahi halali hasa haki miliki za ujuzi za wafanyabiashara wa nchi za nje nchini China ili kuboresha mazingira ya biashara.

    Mwezi Julai mwaka huu, Shirika la Fedha la Kimataifa lilitoa ripoti ya mwaka 2018 kuhusu uchumi wa China, na kusema mageuzi ya China yamepiga hatua katika sekta kadhaa muhimu, na uchumi wa China utaendelea kukua kwa haraka. Mkutano huo wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China pia umefahamisha mwelekeo wa uchumi, na kuonesha imani ya viongozi wa China kuhusu maendeleo ya uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako