• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Wayne Rooney afunguka mazito dhidi ya Jose Mourinho

  (GMT+08:00) 2018-12-25 09:02:16

  Baada ya ukimya wa muda mrefu aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Wayne Rooney amefunguka na kusema anaamini kuwa wafanyakazi wengi wa timu hiyo hawakuwa na furaha na Jose Mourinho. Rooney anaamini kocha mpya wa timu hiyo, Solskjaer ndiye mtu sahihi atakayeweza kubadilisha upepo mbaya wa Old Trafford huku akisema kuwa si kwa wachezaji pekee bali hata kwa klabu nzima. Ole Gunnar Solskjaer amechaguliwa kurithi nafasi ya Mourinho kwa muda na kwa mara ya kwanza amekiongoza kikosi cha United kwenye ushindi wa mabao 5 – 1 dhidi ya Cardiff. Rooney anaamini ni wakati muhimu sasa kuwarudisha wachezaji kuwa wamoja ili kufurahia soka na kumfanya kocha, Solskjaer kukirejesha kikosi hiko kwenye makali yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako