• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka nchi mbalimbali kuheshimu mamlaka na sheria za China

    (GMT+08:00) 2018-12-25 09:39:52

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying akizungumzia kuhusu kitendo cha Canada cha kuwahimiza washirika wake kuonesha ufuatiliaji juu ya China kuwashikilia raia wake wawili, amesema China inapinga kithabiti kauli zilitolewa na baadhi ya nchi zikiwemo Canada na Marekani, pia inazihimiza nchi husika ziheshimu kihalisi mamlaka ya sheria ya China.

    Bibi Hua amesema China inawashikilia raia wawili wa Canada Bw. Michael Kovrig na Bw. Michael Spavor kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za kuhujumu usalama wa China. Idara husika za China zimehakikisha haki zao halali na kutoa msaada wa lazima kwa ubalozi wa Canada kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya kibalozi.

    Pia amesisitiza kuwa vitendo husika vya Marekani na Canada vinapingwa vikali duniani. Amesema China inaihimiza Canada kwa mara nyingine tena kujisahihisha makosa na kumwachia huru Bibi Meng Wanzhou mara moja, na kulinda kihalisi haki zake halali. Vilevile inaihimiza Marekani ifute mara moja amri ya kumkamata Bibi Meng.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako