• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazihimiza baadhi ya nchi kuwa na mtizamo wa haki kuhusu hatua za kulinda utulivu mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2018-12-25 09:58:02

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amewahimiza maofisa na vyombo vya habari vya baadhi ya nchi za magharibi kuachana na upendeleo wa kiitikadi, na kuwa na mtizamo wa haki kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali ya Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur katika kulinda amani na utulivu mkoani humo.

    Bibi Hua Chunying amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana wakati akikanusha habari zilizoripotiwa na Gazeti la Wall Street Journal la Marekani zikisema mwaka mmoja uliopita, China iliongeza nguvu katika kuwasimamia, kuwashikilia na kuwabadilisha waislamu katika mkoa wa Xinjiang, huku ikieneza hatua hizo kwenye sehemu nyingine za waislamu. Bibi Hua amesema hayo ni makosa ya kimsingi ya kupotosha juhudi za China za kupambana na ugaidi na itikadi kali mkoani Xinjiang, kuwa ni vitendo maalumu dhidi ya wauygur au waislamu.

    Amesisitiza kuwa China inapinga kithabiti vitendo vya kupotosha juhudi za China za kupambana na ugaidi na itikadi kali, na kushambulia sera ya China kuhusu makabila na dini bila msingi wowote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako