• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 429 wapoteza maisha kutokana na mlipuko wa Volkano na Tsunami na maelfu kukosa makazi magharibi mwa Indonesia

    (GMT+08:00) 2018-12-25 18:56:05

    Idadi ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa volcano na tsunami katika fukwe wa bahari ya Sunda magharibi mwa Indonesia yaongezeka na kufikia 429 na wengine 1,459 wakijeruhiwa.

    Kwa mujibu wa msemaji wa kitengo cha maafa cha taifa nchini humo, Tsunami imetokea jumamosi usiku kutokana na maporomoko ya ardhi chini ya bahari baada ya kulipuka kwa volkano ya Anak Krakatau na kuharibu vibaya nyumba 882, hoteli na majengo yaliyopo pembezoni mwa fukwe wa bahari huku watu 16,082 wameathirika.

    Zaidi ya askari 2,000 pamoja na polisi wameshirikiana na vikosi vya utafutaji na uokoaji na watu wa kujitolea katika zoezi la uokoaji.

    Mlima Anak Krakatau unaozungukwa na vituo kadhaa vya utalii, eneo la viwanda, njia kubwa ya meli na maeneo mengine ya makazi imekuwa na tahadhari wakati wa Tsunami.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako