• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano na Afrika wapaswa kulingana na matakwa ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-12-25 19:54:39

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, jumuiya ya kimataifa ikifanya ushirikiano na Afrika inapaswa kusikiliza zaidi sauti ya Afrika, na kuamini busara ya Afrika na kuheshimu matakwa ya Afrika.

    Bibi Hua amesema, katika miaka ya hivi karibuni, mafanikio makubwa yamepatikana katika ushirikiano halisi kati ya China na Afrika ambayo yameonesha nia dhati ya wachina kwa waafrika. Ushirikiano huo umekaribishwa na watu wa Afrika na kusifiwa na jumuiya ya kimataifa.

    Pia amesema, China inaendelea kusisitiza kwamba, nchi na watu wa Afrika wana haki na uwezo wa kuchagua wenzi wa ushirikiano. Matusi yasiyojali hali halisi ya ushirikiano kati ya China na Afrika hayatakubaliwa na pande ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako