• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya na China zaendelelea kukuza ushirikiano wa kunufaishana

  (GMT+08:00) 2018-12-26 08:46:51

  Ushirikiano wa China na Kenya Mwaka wa 2018 umendelea kupiga hatua mpya ukifaidi watu wa pande hizo mbili.

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezuru China mara mbili mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine yeye na mwezake wa China Xi Jinping walisaini makubaliano ya kibiashara.

  Sasa mwandishi wetu Jacob Mogoa anaripoti kuhusu ushirikiano na mafanikio yalipatikana.

  Mwaka wa 2018 ulikuwa ni mwaka ambao hautasahaulika kamwe unapozaungumzia ushirikiano kati ya China na Kenya.

  Septemba mwaka huu rais Uhuru Kenyatta aliandama na ujumbe wake hadi mjini Beijing kuhudhuria mkutano wa Focac ambako alifanya mazungumzo na rais Xi Jinping kuhusu miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na China nchini Kenya.

  Kwenye mkutano huo rais Xi Jinping alitoa hatua mpya za kuhimiza ushirikiano katika sekta nane za uzalishaji, miundo mbinu, biashara, maendeleo yasiyosababisha uchafuzi, ujenzi wa uwezo, afya, mawasiliano ya watu, na usalama.

  Akizungumzia hatua hizo, rais Uhuru Kenyatta wa alisema hatua hizo ni mafanikio makubwa zaidi yaliyofikiwa kwenye mkutano huo, kwani imepanga njia halisi ya maendeleo ya pamoja ya China na Afrika.

  Alisema Kenya inapania kutumia nafasi hiyo kuboresha miundo mbinu yake ikiwemo barabara, reli na kadhalika.

  "Baadhi mambo muhimu ambayo tulifuatilia katika kipindi cha kwanza ilikuwa ni ujenzi wa miundo mbinu kama vile ujenzi wa reli, barabara na kadhalika , lakini hivi sasa tunalenga zaidi mambo kama afya, nyumba na makazi, ajira haya ndio mambo ambayo tunashughulikia kwa sasa na tuna imani kuwa tutaiweka nchi yetu kwa hatua nyingine".

  China na Kenya zimekuwa zikifanya majadiliano kuhusu siasa, uchumi na biashara pamoja na usalama.

  Hata hivyo katika siku za hivi karibuni Kenya imekuwa ikijenga miundo mbinu yake kama vile barabara, reli na madaraja kwa kushirikiana na China ili kurahisisha sekta ya usafiri ambayo ilikuwa imesambaratika. Wachina huamini kuwa ni vyema kumfundisha mtu kuvua samaki, badala ya kumpa samaki.

  Mbali na kutoa mafunzo wakati wa kujenga reli ya SGR, kampuni ya ujenzi ya China ambayo ilijenga reli hiyo imekuwa ikizingatia sana kuwafundisha wenyeji wanaoendesha na kusimamia reli hiyo.

  Katika hali hiyo mawasiliano ya watu wa pande zote mbili yalionekana kukumbatiwa. Baadhi ya wafanyi kazi waliozungumza na radio China walionyesha furaha yao baada ya kupata ujuzi wa kikazi kutoka kwa ndugu zao wachina.

  Ushirikiano huu wa Kenya na China pia ulionekana kukata maini nchi za magharibi nyingi zikidai kuwa China inalenga kuzilimaza nchi za Afrika na madeni.

  Hata hivyo akizungumza na shirika la habari la Marekani CNN rais Uhuru Kenyatta alisimama kidete na China na kusisitiza kuwa China mshirika wake muhimu sawa na nchi nyingine .

  Akizungumzia suala hilo, balozi wa China nchini Kenya Bi Sun Baohong nia ya China ni kuhakikisha Afrika inapiga hatua kwenye maendeleo ya kiuchumi sawa na nchi nyingine zilizostawi.

  "Mtego wa madeni sio jambo la kufikiriwa kwa ndugu zetu wa Afrika.Ni wazo la magharibi. Afrika inataka kujiendeleza na ukiangalia mipango ya maendeleo ambayo imewekwa na umoja wa Afrika hasa miundo mbinu inaonyesha kuwa Afrika inahitaji karibi bilioni 900 ili kujenga miundo mbinu pekee".

  Kwa miaka mitatu mfululizo , China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Kenya, mwekezaji na pia mjenzi wa miundo mbinu. Kuna jumla ya makampuni 400 ya kichina nchini Kenya ambayo yametoa jumla ya ajira 130,000 kwa wakenya.

  Vile vile wakenya wengi wamepata mafunzo kupitia ujuzi waliopata kwenye kampuni hizo za wachina huku wengine wakipelekwa China kwa mafunzo zaidi.

  Hivi sasa thamani ya biashara kati ya China na Afrika inakisiwa kuwa zaidi ya dola bilioni 5.2 za Marekani huku ile ya Afrika ikiwa zaidi ya bilioni 170.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako