• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Jermain Defoe apewa tuzo baada ya kupita miaka kumi

  (GMT+08:00) 2018-12-26 10:22:01

  Waratibu wa Kombe la Ligi nchini England, wamemtuza mshambuliaji nguli wa nchi hiyo, Jermain Defoe, ikiwa imepita miaka kumi tangu aipatie Tottenham ubingwa. Defoe alifunga bao karibu kila mchezo kuanzia raundi ya kwanza hadi nusu fainali akiitumikia Spurs mwaka 2008 lakini akauzwa kwenda Portsmouth wiki chache kabla ya mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Wembley ambako walitwaa ubingwa. Kwa kutoshiriki mchezo wa fainali ambao Spurs iliifunga Chelsea mabao 2-1, Defoe hakupata medali wala tuzo yoyote lakini miaka kumi baadaye Chama cha soka kimebaini alistahili tuzo kutokana na kutoa mchango mkubwa unaostahili kuenziwa. Mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa anaitumikia Bournemouth, ndiye aliyefunga bao lililoing'oa Manchester City katika nusu fainali ya michuano hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako