• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la Syria lafanikiwa kuzuia makombora ya Israel kwenye anga ya Damascus

  (GMT+08:00) 2018-12-26 20:33:13

  Vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria jana jioni vilifanikiwa kuzuia makombora ya Israel yaliyokuwa yakilenga maeneo ya magharibi mwa mji wa Damascus.

  Televisheni ya taifa imesema vikosi vya ulinzi wa anga vilizuia makombora mengi ya Israel kabla hayajafikia kwenye shabaha zake, na kuongeza kuwa ghala moja tu la silaha liliharibiwa na askari watatu walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

  Kwa mujibu wa televisheni hiyo, shambulizi hilo lilitekelezwa kutoka kwenye anga ya Lebanon, na baadhi ya makombora yalizuiliwa yakiwa kwenye anga ya Lebanon.

  Shambulizi hilo la Israel ni jipya kati ya mashambulizi ya mfululizo yanayolenga vituo vya vikosi vinavyoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa Hezbollah nchini Syria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako