• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Ole Gunnar Solskjaer aonesha makali yake Old Trafford

  (GMT+08:00) 2018-12-27 10:22:45

  Kocha wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameaanza kuonesha makali yake katika mchezo wa kwanza wa nyumbani kwa kuondoka kifua mbele kwa kupata magoli 3-1 dhidi ya Huddersfield. Katika mchezo huo Paul Pogba aliisaida timu yake kupachika mabao mawili. Baada ya kupata ushindi wa magoli 5-1 walipocheza dhidi ya Cardiff, kwenye mechi yake ya kwanza tangu achukue nafasi ya Jose Mourinho wikiendi iliyopita Solskjaer ameiwezesha timu yake kupata pointi sita ndani ya siku tano katika kipindi cha Christmas. Goli la kwanza la Solskjaer akiwa Old Trafford limepatikana dakika 28 baada ya Pogba kupiga free-kick. Ole Gunnar Solskjser anakuwa meneja wa tano wa Manchester United, kushinda michezo miwili mfululizo katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu. Makocha wengine waliowahi kufanya hivyo ni Tj Wallworth, Matt Busby, Dave Sexton, na Jose Mourinho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako