• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya kisiasa yasaidia ukuaji wa uchumi na kuleta amani Kenya

    (GMT+08:00) 2018-12-27 10:44:12

    Mwaka 2018 Kenya imeshuhudia maendeleo makubwa ya kisiasa na kufungua ukarasa mpya katika kukuza amani, mashikamano na kukabiliana na migawanyiko ya kikabila.

    Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walifanya makubaliano ya kuacha uhasama na kufanya kazi pomoja kwa ajili ya kuleta maendeleo ya kiuchumi nchini humo.

    Jacob Mogoa anaripoti kutoka Nairobi.

    Baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya mwaka 2017, kulikuwa na mvutano wa kisiasa kati ya chama tawala nchini humo na muungano wa upinzani NASA.

    Maandamano ya wafuasi wa upinzani dhidi ya serikali yalitatiza shughuli za kila siku.

    Na hata kiongozi wa upinzani nchini humo akajiapisha kwenye bustani ya Uhuru.

    Lakini baada ya miezi miwili ya misimamo mikali, Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walifanya mkutano Machi 5 katika jumba la Harambee.

    Kwenye mkutano huo wawili hao walikubaliana kuundwe mpango wa pamoja wa kuangazia utekelezaji wa malengo ya pamoja.

    Walikubaliana pia kuunda kamati ya kutafuta njia za kukewa uwiano baina ya makabila nchini Kenya na kukuza umoja wa kitaifa.

    Ilikuwa ni afueni kwa wakenya wengi.

    "Watu wa hapa ambao ni wajaluo walikuwa hawapendi kuuzia wagikuyu ardhi, lakini sasa wameanza kuwauzia baada ya viongozi kusalimiana"

    Tangu viongozi hao wawili wafanye makubaliano, wamekuwa wakifanya mikutano mingi kwa pamoja ili kuhimiza wakenya kuishi na amani na kutojali tofauti za kisiasa baina yao.

    Rais Uhuru Kenyatta anaona kwamba ushirikiano kati yake na upinzani ndio njia ya pekee ya kuondoa uhsama wa kila badaa ya miaka mitano kati ya wafuasi mbalimbali wa kisiasa.

    "Tulikaa pamoja na tukasema yaliopita si ndwele, tugange yajayo. Hatuwezi tena kusema sisi ni viongozi lakini kila baada ya miaka mitano, wakenya wanamwaga damu ati kwa sababu ya kuchagua viongozi. Lazima tuketi na tujiulize shida iko wapi. Tujiulize ni kwa nini siasa yetu imekuwa ya ukabila na matusi"

    Katika Muungano wa National Super Alliance (Nasa) ambao ulibuniwa mwaka jana, Bw Odinga alikuwa na viongozi wengine wa vyama vya upinzani, hususan makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka ambaye ni kiongozi wa chama cha Wiper Democratic Movement of Kenya Musalia Mudavadi wa Amani National Congress (ANC) na Moses Wetangula wa chama cha Forum for the Restoration of Democracy-Kenya (Ford-Kenya).

    Na sasa wote wanamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta katika azma ya serikali ya kuleta maendeleo .

    Rais Uhuru Kenyatta anaona makubaliano pande mbili kama mafanikio makubwa na ya kihistoria.

    "Kwa mara ya kwanza kwa historia ya taifa leu la Kenya, tangu tupate uhuru, viongozi wa vyama vikubwa viwili vya Kenya NASA na Jubilee walisimama pamoja, kusherehekea sikukuu ya jamhuri pamoja tulionyesha kukomaa kwa siasa yetu, na hapo ndio sisi tungependa kuendelea"

    Matunda ya uwiano na makubaliano ya kisiasa nchini Kenya yalianza kuoneakana baada ya Raola Odinga kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika mswala ya miundo mbinu.

    Kazi zake zitakuwa ni pamoja na kujadiliana na wafadhili, kutafuta ungwaji mkono wa miradi kutoka nchi wanachama na kuongoza juhudi za kuboresha miundo msingi barani humo.

    Anaona kuwa amani, na utulivu wa kisiasa nchini Kenya sio tu kwa manufaa ya nchi hiyo lakini pia na kwa kanda ya Afrika Mashariki.

    "Mimi na rais tuliamua turejeshe Kenya mahali ilikuwa mwaka 1963 wakati tulipata uhuru. Tupigane na ukabila, tupigane na ubaguzi, ufisadi, na tuunganishe Kenya pamoja. Tumeamua pia sio kuunganisha Kenya tu lakni pia na Afrika Mashariki na Afrika yote kwa jumla. Na juzi mimi niliulizwa na mkuu wa Umoja wa Afrika niwe mwakilishi wa Umoja huo katika mswala ya miundo mbinu, na nimekubali"

    Naye Kalonzo Musyoka ambaye alikuwa mgombea mweza wa Raila Odinga aliteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuwa mwakilishi wa wa maswala ya amani ya Sudan Kusini chini ya muungano wa maendeleo Afrika Mashariki na pembe ya Afrika (IGAD).

    Aidha kuboreka kwa mazingira ya kisiasa nchini humo kumechangia imani ya wawekezaji, kuimarika kwa shilingi dhidi ya dola na ukuaji wa uchumi.

    Kulingana mwenyekiti wa chama cha wafanyabishara nchini Kenya Kiprono Kittony, anasema sasa kampuni nyingi zimeanza kuzalisha faida na kupata ongezeko la mauzo tangu makubaliano ya kisiasa yafanyike.

    Nayo benki ya dunia imetabiri kuwa mwaka 2018, uchumi wa Kenya utakua kwa asilimia 5.5 ikilinganishwa na makadirio ya ukuaji wa awali wa asilimi 4.6 tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako