• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu yahimiza maendeleo yenye ubora zaidi nchini China

    (GMT+08:00) 2018-12-27 17:10:24

    Huu ni mwaka wa 30 tangu China ianze kujenga maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu. Katika miaka 30 iliyopita, maeneo hayo yameendelea kwa kasi, na kutoa matokeo mengi ya teknolojia na bidhaa mpya.

    Ujenzi wa maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu ni mpango mkubwa wa kimkakati wa serikali ya China kwa ajili ya kuhimiza mageuzi na kufungua mlango. Tarehe 10 Mei mwaka 1988, baraza la serikali la China liliidhinisha kujenga eneo la kwanza la majaribio la sekta ya teknolojia mpya mjini Beijing, ambalo sasa linajulikana kama eneo la sayansi na teknolojia la Zhongguancun. Waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Wang Zhigang amesema, hadi sasa baraza la serikali la China limeidhinisha kujenga maeneo 168 ya ngazi ya kitaifa ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu. Anasema,

    "Mwaka 1991, mapato ya maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu yalikuwa yuani bilioni 8.73, na mwaka jana mapato hayo yalifikia yuani trilioni 33.2. Na kiwango cha mapato hayo katika mapato yote ya taifa la China kiliongezeka kutoka asilimia 2.6 ya mwaka 2001 hadi 11.5 ya mwaka 2017."

    Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Tangu yaanze kujengwa, maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu yametoa mchango muhimu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii. Bw. Wang anasema,

    "Kwanza ni kuzidisha mawazo ya "serikali ndogo, huduma kubwa", na kuhimiza kujenga idara za usimamizi zenye ufanisi mkubwa. Pili ni kusukuma mbele juhudi za kuboresha mazingira ya kibiashara. Na tatu ni kufanya uvumbuzi wa sera na majaribio ili kupata uzoefu unaoweza kutekelezwa katika sehemu nyingine."

    Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, mageuzi ya China yanakabiliwa na hali ya kutatanisha zaidi, na uvumbuzi umekuwa mkakati wa kitaifa. Naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Xu Nanping amesema, maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu yatajijenga kuwa maeneo ya vielelezo vya uvumbuzi na maendeleo yenye ubora zaidi. Anasema,

    "Katika zama mpya, kazi kuu ya maeneo ya sekta ya teknolojia mpya na za hali ya juu ni kuendeleza teknolojia za hali ya juu, na kuzitumia kibiashara, na kuyajenga kuwa maeneo yenye uvumbuzi ustawi na maendeleo yenye ubora zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako