• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kufanya maandalizi ya mawasiliano kati ya viongozi wa China na Russia

    (GMT+08:00) 2018-12-27 18:59:49

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, mwaka kesho utakuwa na maadhimisho ya miaka 70 tangu China na Russia zianzishe uhusiano wa kibalozi. Pande mbili zitaendelea kushirikiana na kufanya maandalizi vizuri ya mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili hasa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili.

    Bibi Hua Chunying amesema, msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zhang Hanhui amefanya mazungumzo na naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Igor Morgulov, na kubadilishana maoni kuhusu mpango wa mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

    Habari zinasema, balozi wa Russia nchini China Bw. Andrey Denisov jana amesema, rais Vladmir Putin wa Russia atahudhuria mkutano wa pili wa baraza la ngazi ya juu la ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja na Njia moja", na rais Xi Jinping wa China atafanya ziara nchini Russia mwakani pia. Na Mawaziri wakuu wa China na Russia watakutana mapema mwaka kesho nchini Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako