• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Olimpiki: Mwenyekiti wa zamani wa NOCK afariki dunia

  (GMT+08:00) 2018-12-28 08:57:12

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Taifa ya Kenya (NOCK) Charles Mukora amefariki dunia jana jioni. Bw. Mukora aliyekuwa mjumbe wa IOC pia alikuwa kocha wa riadha ambaye aliwafunza wanariadha wengi tajika akiwemo Kipchoge Keino. Mukora aliachia ngazi kama mwenyekiti wa NOCK mwaka 1999 baada ya kutuhumiwa kwa kutumia fedha vibaya alipoizawadia Salt Lake City michezo ya Majira ya baridi ya mwaka 2002 na michezo ya majira ya joto ya mwaka 2000 kuipa Sydney. Hata hivyo alikanusha madai yote hayo lakini alikubali kuacha kazi kama afisa wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC na NOCK baada ya kutakiwa na rais wa wakati huo wa IOC Juan Antonio Samaranch.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako