• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masumbwi: Dullah Mbabe amdundaFrancis Cheka kwa Knock Out

    (GMT+08:00) 2018-12-28 08:57:31

    Siku ya Boxing Day viwanja vya PTA Sabasaba mabondia Dullah Mbabe na Francis Cheka walipanda ulingoni kuonesha ubabe, katika pambano hilo la uzito wa kati (Middleweight), Dullah Mbabe alifanikiwa kumpiga Francis Cheka kwa Knock Out (KO) round ya 6 ya pambano lililokuwa la raundi 12 na kutangazwa Bingwa wa WBF. Baada ya kudundwa bondia Francis Cheka alidai kipigo chake hakijasababishwa na umri au kiwango chake kushuka isipokuwa mpinzani wake alimuotea tu na kushinda. Amesema hadi sasa hajajua amepotezaje pambano hilo, lakini pamoja na kupoteza hawezi kustaafu ngumi kwa sasa. Hata hivyo Dullah Mbabe Ametamba kwamba kipigo hicho kwa Cheka si cha kubahatisha alijiandaa kumnyamazisha bondia huyo bingwa wa zamani wa dunia wa WBF.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako