• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa utambuzi wa mahali wa Beidou No. 3 wa China waanza kutoa huduma kwa dunia nzima

    (GMT+08:00) 2018-12-28 16:29:34

    Msemaji wa mfumo wa utambuzi wa mahali kupitia satalaiti wa Beidou No. 3 wa China Bw. Ran Chengqi ametangaza kuwa, mfumo huo umekamilika kimsingi, na kuanza kutoa huduma kwa dunia nzima.

    Mfumo wa Beidou ni mfumo wa utambuzi wa mahali kupitia satalaiti uliojengwa na kuendeshwa na China kwa kujitegemea, na unaweza kushirikiana na mifumo mingine ya aina hiyo duniani. Tangu utafiti uanze kufanya kazi katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, China imemaliza ujenzi wa mifumo ya Beidou No.1, No.2 na No. 3. Mkurugenzi wa ofisi ya uendeshaji wa mifumo ya utambuzi wa mahali kupitia satalaiti ya China, ambaye pia ni msemaji wa mfumo wa Beidou No. 3 Bw. Ran Chengqi jana alitangaza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa kimsingi wa Beidou No.3 kunamaanisha kuwa mfumo huo umeingia katika kipindi cha kutoa huduma kwa dunia nzima. Anasema,

    "Natangaza kuwa, mfumo wa Beidou No.3 umekamilika kimsingi, na kuanzia leo kutoa huduma kwa dunia nzima. Tathmini ya upimaji inaonesha kuwa usahihi wa utambuzi wa mahali duniani kote ni mita 10, na katika ukanda wa Asia na Pasifiki, unaweza kufikia mita 5. Nchi zote duniani zikiwemo zile zinazohusika na Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' zinaweza kutumia huduma za mfumo huo."

    Bw. Ran amesema, ikilinganishwa na mifumo mitatu ya utambuzi wa mahali kupitia satalaiti duniani ikiwemo GPS wa Marekani, Glonass wa Russia na Galileo wa Umoja wa Ulaya, mfumo wa Beidou unashika nafasi ya mbele katika ukubwa wa maeneo yanayofunikwa na ubora wake, na kupiga hatua katika teknolojia nyingi muhimu, anasema,

    "Tangu siku ya kwanza tulipoanza kujenga mfumo wa Beidou, teknolojia kuu zimetafitiwa na wafanyakazi wetu wenyewe. Tumefanya uvumbuzi kwa wingi, kwa mfano njia ya mawasiliano kati ya satalaiti, na saa za kiatomiki."

    Bw. Ran pia amesisitiza kuwa, ili kuhakikisha wateja wanapata huduma bora zaidi, licha ya kutoa huduma za kawaida kwa dunia nzima, mfumo wa Beidou pia utabakiza na kuboresha huduma maalumu za kupokea na kutuma ujumbe.

    Kuanza kutoa huduma kwa dunia nzima ni hatua kubwa ya ujenzi wa mfumo wa Beidou wa China, na pia ni mwanzo mpya wa mfumo huo. Bw. Ran amesema, mfumo huo utaongeza ubora wake hatua kwa hatua, ili kutoa huduma nzuri zaidi wa binadamu. Anasema,

    "Hadi kufikia mwaka 2020, China itarusha satalaiti 11 nyingine za Beidou No.3 na moja ya Beidou No. 2, ili kukamilisha ujenzi wa mfumo huo na kutoa huduma bora zaidi. Na hadi kufikia mwaka 2035, China itakamilisha ujenzi wa mfumo wa utambuzi wa mahali na uthibitishaji wa wakati, kupitia Satalaiti."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako