• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Barcelona yamngángánia mlinda mlango Jasper Cillessen

  (GMT+08:00) 2018-12-31 08:56:13

  Klabu ya Barcelona imesema mlinda mlango, Jasper Cillessen, hataruhusiwa kuondoka chini ya euro milioni 60. Cillessen alikuwa na ofa kutoka klabu za Ligi Kuu ya England majira ya joto yaliyopita, lakini akashawishika kubakia na kupigania nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza na Marc-Andre ter Stegen. Barcelona bado ina msimamo wa kutomruhusu Cillessen kuondoka na hivyo haitazingatia ofa yoyote chini ya euro milioni 60 itakayotolewa katika mkataba wake. Real Madrid na Barcelona nao ni miongoni mwa klabu zilizotoa ofa kwa ajili ya beki wa kati wa Toulouse, Jean-Clair Todibo. Todibo ambaye juzi alifikisha umri wa miaka 19, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo ya 'Ligue 1' huku mkataba wake ukimalizika mwishoni mwa msimu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako