• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riadha: Dibaba na Obiri kukwaana kwenye mbio za San Silvestre Vallecana za Madrid

  (GMT+08:00) 2018-12-31 08:57:46

  Mbio za San Silvestre Vallecana za Madrid kwa mara nyingine tena zinawakutanisha wakimbiaji nguli duniani kwa wanawake na wanaume ambazo zinafanyika leo December 31. Mbio hizi zinazofanyika kila Disemba 31 kwa wanawake zinawaleta pamoja barabarani mkimbiaji tajika wa Ethiopia Tirunesh Dibaba na Wakenya Hellen Obiri na Brigid Kosgei. Dibaba, ambaye ni bingwa mara nyingi wa Olympic na dunia, hivi sasa ana miaka 33 na katika miaka zaidi ya miwili iliyopita alijihusisha zaidi na marathon. Dibaba atakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Wakenya kama vile Obiri, mtaalamu wa mita 1,500 aliyepata medali ya shaba mwaka 2013 katika mbio za mabingwa wa dunia, na kufanya vizuri katika mbio za mabingwa mita 5000 akiandikisha muda mzuri wa 14:18:37. Mbio hizo zitakuwa za Kilomita 10 na zitaanza kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu wa Real Madrid na kumalizikia kwenye uwanja mwingine wa timu ya soka ya Rayo Vallecano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako