• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba ya kukaribisha mwaka mpya wa 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-31 19:29:11

    Makomredi, marafiki, mabibi na mabwana,

    Hamjambo! "Wakati hausimami, na msimu hutiririka kama maji". Mwaka 2019 unawadia, na mimi niko hapa Beijing kuwatakia ninyi nyote kila la heri.

    Katika mwaka 2018 tulitembea kwa uimara na kupata mafanikio mengi. Mwaka huu, tumeshinda changamoto mbalimbali katika kuhimiza maendeleo yenye ubora zaidi, kuharakisha mabadiliko ya injini ya uchumi na kuhakikisha uchumi unaendelea kwa kasi inayofaa. Wakati huo huo, juhudi za kulinda usafi wa hewa, maji, na ardhi zimepiga hatua, shughuli za huduma za jamii ziliendelea kuhimizwa, na maisha ya watu yameboreshwa kwa mfululizo. Aidha, mikakati ya kitaifa ya maendeleo ya pamoja ya miji ya Beijing na Tianjin na mkoa wa Hebei, maendeleo ya uchumi wa ukanda wa Mto Changjiang, na ujenzi wa eneo la kiuchumi la ghuba kubwa ya Guangdong, Hongkong na Macao. Nilipofanya ukaguzi, nilifurahia kuona rangi ya kijani kando ya Mto Changjiang, hekta 1,100 za mpunga katika sehemu ya Jiansanjiang, bandari yenye ustawi ya Qianhai ya Shenzhen, eneo la teknolojia ya juu ya la Zhangjiang mjini Shanghai, na daraja kubwa linalounganisha Hongkong, Zhuhai na Macao. Mafanikio haya yamepatikana kutokana na juhudi kubwa za watu wa makabila yote ya China, ambao ni wajenzi wa zama mpya.

    Mwaka huu, tumepiga hatua katika uzalishaji, uvumbuzi na ujenzi, na kuendelea kubadilisha sura ya China. Tulifanikiwa kurusha chombo cha uchunguzi cha Chang'e No. 4, kujaribu manowari ya pili ya kubeba ndege za kijeshi, kurusha ndege kubwa ya kutumika angani na majini inayotengenezwa na sisi wenyewe kwa mara ya kwanza, na kufanikisha mfumo wa utambuzi wa mahali wa Beidou uanze kutoa huduma kwa dunia nzima. Hapa nataka kuwashukuru wanasayansi, wahandisi, "mafundi wakubwa", wajenzi na watu wengine wote walioshiriki kwenye miradi hiyo.

    Mwaka huu, pia tumepata mafanikio mengi katika mapambano dhidi ya umaskini. Wilaya nyingine 125 na watu wengine milioni 10 vijijini wameondokana na umaskini. Pia tumeweka aina 17 za dawa dhidi ya saratani katika bima ya matibabu, ili kuondoa umaskini unaotokana na magonjwa. Mara kwa mara nawakumbuka makomredi wetu walioko mstari wa mbele wa kupambana na umaskini, watu hao zaidi ya milioni 2.8 wakiwa maofisa na makatibu wa kwanza vijijini wanafanya kazi kwa bidii, tafadhali mjitunze vizuri.

    Siku zote nakumbuka watu maskini. Katika kijiji cha Sanhe cha wilaya ya Liangshan mkoani Sichuan, nilitembelea familia za Jihao Yeqiu na Jilie Eamu wa kabila la Wayi. Katika kijiji cha Sanjianxi cha mji wa Jinan mkoani Shandong, niliongea na watu nyumbani mwa Zhao Shunli. Katika mtaa wa Donghuayuan wa mji wa Fushun mkoani Liaoning, nilimtembelea Chen Yufang ili kujua hali yake ya kuhama kutokana na ubovu wa nyumba. Katika kijiji cha Lianzhang ya mji wa Qingyuan mkoani Guandong, niliongea na mtu maskini Lu Yi kuhusu mpango wa kuondokana na umaskini. Wakati wa kufika kwa mwaka mpya, nawatakia wanavijiji wote maisha bora.

    Mwaka huu, tuliadhimisha miaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, tulifanya marekebisho makubwa ya mifumo, ujumla na mwundo mpya katika idara za chama na serikali, tuliandaa maonesho ya kwanza ya kimataifa ya bidhaa zinazoingizwa na China kutoka nchi za nje, na tulianzisha eneo la majaribio la biashara huria la mkoa wa Hainan. Dunia imegundua kasi ya China ya kufungua mlango zaidi, na nia yake ya kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango mpaka mwisho. Hatutasimamisha mageuzi, na mlango wetu utafunguliwa zaidi.

    Nimetambua kuwa mwaka huu, kundi la kwanza la watu waliohitimu masomo katika vyuo vikuu tangu kurejea kwa mitihani ya kujiunga na vyuo vikuu wamestaafu, huku wanafunzi wengi waliozaliwa baada ya mwaka 2000 walianza kujiunga na vyuo vikuu. Kazi ya kuwafanya zaidi ya watu milioni 100 waliozaliwa katika sehemu nyingine wawe wakazi wa mijini yanaendelea, na watu milioni 13 wamepata ajira mijini. Tumeanza kujenga nyumba milioni 5.8, kwa ajili ya wakazi wapya walioishi katika makazi duni mijini. Watu wengi wa Hongkong, Macao na Taiwan wamepata kitambulisho cha wakazi wa China bara. Reli ya mwendo kasi ya Hongkong imeunganishwa na mtandao wa reli ya mwendo kasi ya China. Kurahisisha uhamiaji na usafirishaji kumeleta ustawi zaidi kwa China. Sisi sote tunakimbia, na sisi sote tunakimbilia ndoto.

    Wakati huu nataka kutaja majina ya watu kadhaa maalumu. Mwaka huu, nyota moja angani ilipewa jina la Nan Rendong, na pacha za Lin Junde na Zhang Chao zimewekwa kama mashujaa wa mfano wa kuigwa wa majeshi. Pia tunapaswa kukumbuka Wang Jicai aliyelinda visiwa kwa miaka 32, Huang Qun, Song Yuecai na Jiang Kaibin waliopoteza maisha kwa ajili ya kulinda jukwaa la majaribio, na watu wengine waliojitoa mhanga kwa ajili ya taifa na wananchi. Wao ni watu wanaopendwa zaidi katika zama mpya, na tunapaswa kuwakumbuka na kujifuza kutoka kwao daima.

    Mwaka huu, marafiki zetu wengi wapya au wa muda mrefu walitembelea China. Tuliandaa mkutano wa Bo'ao wa Baraza la Asia, mkutano wa kilele wa Qingdao wa Jumuiya ya Ushirikano ya Shanghai, na mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ili kutoa mapendekezo na sauti ya China. Pia mimi na wenzangu tulitembelea nchi mbalimbali za mabara matano makuu duniani, na kuhudhuria shughuli nyingi muhimu za kidiplomasia. Tulifanya mawasiliano mapana na viongozi wa nchi nyingine, tuliimarisha urafiki na uaminifu, na kuongeza marafiki wetu duniani.

    Mwaka 2019 tutaadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Katika miaka hiyo 70 tumekabiliana na changamoto mbalimbali na kupata maendeleo makubwa. Watu ni msingi wa nchi yetu, na pia ni chanzo cha imani cha utawala wetu. Katika miaka hiyo, watu wa China wamefanya kazi kwa bidii na kujitegemea, na kutengeneza mwujiza wa kichina unaoshangaza dunia nzima. Katika siku za baadaye, bila kujali tutakabiliwa na hali ya namna gani, ni lazima tutegemee watu, kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea, na kusukuma mbele shughuli zetu tukufu ambazo hatukufanya zamani hatua kwa hatua kwa nia imara, kwa bidii, na kwa uvumilivu.

    Mwaka 2019 tutakuwa na fursa pamoja na changamoto, na tunapaswa kufanya juhudi kwa pamoja. Sera ya kupunguza kodi inapaswa kutekelezwa vizuri zaidi ili kupunguza mizigo ya kampuni. Pia tunatakiwa kusikiliza sauti za maofisa wa shina, ili kuhamasisha maofisa hodari wanaowajibika wawe na shauku zaidi ya kufanya kazi. Ni lazima tumalize lengo la kuondoa umaskini kwa watu milioni 10 vijijini kwa wakati, kupitia juhudi kubwa. Tunapaswa kuwatendea vizuri wanajeshi waliostaafu, kwani wametoa mchango kwa ajili ya ulinzi wa taifa letu. Wakati huu, mamilioni ya wafanyakazi wakiwemo wapeleka vifurushi, wasafanya usafi na madereva wa taksi bado wanaendelea na kazi, tunapaswa kuwashukuru watu hao wanaotengeneza uzuri kwa ajili ya maisha yetu. Poleni na kazi!

    Tukitupia macho duniani, tunanaona kuwa tunakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika miaka 100 iliyopita. Lakini bila kujali kuna mabadiliko gani duniani, imani na nia ya China ya kulinda mamlaka na usalama wa taifa haitabadilika, na udhati na wema wa China wa kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja hautabadilika. Tutaendelea kusukuma mbele ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa hatua madhubuti, kuhimiza kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, na kufanya juhudi kwa ajili ya kujenga dunia yenye ustawi na uzuri zaidi.

    Kengele ya mwaka mpya italia, tafadhali tuukaribishe pamoja mwaka wa 2019 kwa imani na matumaini.

    Naitakia China kila la heri! naitakia dunia kila la heri!

    Asanteni!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako