• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Guardiola asema Liverpool inaweza kuwa timu bora zaidi duniani kwa sasa

  (GMT+08:00) 2019-01-01 09:09:22

  Pep Guardiola anasema kuwa Manchester City lazima ikubali kwamba wapinzani wake wakuu katika ligi ya Uingereza Liverpool wanaweza kuwa timu bora zaidi duniani kwa sasa. Mabingwa watetezi City, ambao waliishinda Southampton, wanashiriki katika mechi ya siku ya Alhamisi dhidi ya Liverpool wakiwa alama saba nyuma ya viongozi hao wa ligi.

  Huku City ikiwa imeshindwa mara kadhaa dhidi ya Chelsea, Crystal Palace na Leicester mwezi Disemba, Liverpool imeshinda mechi zake zote saba za ligi walizocheza. Walimaliza mwaka 2018 kwa bashasha baada ya kuifunga Arsenal 5-1 katika uwanja wa Anfield na hivyo basi kupanda kwa alama 10 dhidi ya City kwa muda. Iwapo Liverpool itashinda siku ya Alhamisi wataimarisha alama zao 10 juu ya jedwali la ligi na wanapigiwa upatu kushinda taji la ligi tangu 1990.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako