• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ndondi: Floyd Mayweather mdunda mpinzani wake wa Japan Tenshin Nasukawa

  (GMT+08:00) 2019-01-01 09:10:46

  Imemchukua sekunde 140 pekee kwa Floyd Mayweather kumshinda mpinzani wake wa Japan Tenshin Nasukawa katika pigano la maonyesho lililokuwa na thamani ya dola $9m. Mayweather ambaye ni bingwa mara tano wa zamani mwenye umri wa miaka 41 alikuwa akitabasamu wakati wa pigano hilo la muda mfupi mjini Tokyo alipombwaga mara tatu mpinzani wake mwenye umri wa miaka 20. Pigano hilo la raundi tatu lilimalizika huku Nasukawa akibubujikwa na machozi baada ya kikosi chake kurusha kitambaa cheupe ndani ya ulingo kikitaka pigano kusitishwa. Licha ya kurudi katika pigano hilo Mayweather alisema yeye amestaafu ndondi za kulipwa. Mabondia wote wawili hawakuwahi kushindwa kabla ya pigano hilo lililokosolewa ambapo Mayweather alikua na uzani wa juu wa kilo 4 dhidi ya mpinzani wake. Kwenye shindano hilo hakukuwa na majaji huku Knockout ikiwa ndio ushindi. Kabla ya pigano hilo bingwa wa zamani katika uzani wa Super Lightweight Amir Khan alisema kuwa pigano hilo ni ''mzaha mkubwa''.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako