• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Fanya kazi kwa bidii, kimbia kwa kasi ya kichina

  (GMT+08:00) 2019-01-01 10:39:40

  Rais Xi Jinping wa China jana alitoa hotuba ya kukaribisha mwaka mpya, akifanya majumuisho ya mafanikio ya China katika mwaka 2018, na kuwahamasisha wachina wote kuendelea kuchapa kazi ili kutimiza ndoto, na pia kueleza udhati na wema wa China katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja duniani.

  Kwenye hotuba yake, rais Xi amefanya majumuisho ya mafanikio ya China katika uchumi, uhifadhi wa mazingira, maisha ya watu, uvumbuzi, mageuzi na kufungua mlango, na kusisitiza kuwa mafanikio hayo yanatokana na juhudi kubwa za wachina wakiwa wajenzi wa zama mya. Amesema mwaka 2018, China iliwasaidia watu milioni 10 kuondoka na umaskini, na kujenga nyumba milioni 5.8 kwa ajili ya watu wanaoishi katika makazi duni.

  Huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na pia ni mwaka muhimu kwa juhudi za kujenga jamii yenye maisha bora. Rais Xi amesema China itakuwa na fursa pamoja na changamoto, na wachina wanapaswa kufanya juhudi kwa pamoja. Amesema sera ya kupunguza kodi inapaswa kutekelezwa vizuri zaidi ili kupunguza mzigo kwa makampuni, na lengo la kuondoa umaskini kwa watu milioni 10 vijijini pia linatakiwa kutimizwa kwa wakati.

  Aidha, rais Xi amesema bila kujali kuna mabadiliko gani duniani, imani na nia ya China ya kulinda mamlaka na usalama wa taifa haitabadilika, na udhati na wema wa China wa kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja hautabadilika. Kauli hii imeonesha nia ya China ya kuwajibika ikiwa nchi kubwa duniani, na pia kuonesha nia ya rais Xi ya kuchangia amani na maendeleo duniani akiwa kiongozi wa nchi kubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako