• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Salah, Sadio Mane na Aubameyang kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika (CAF)

  (GMT+08:00) 2019-01-02 09:04:38

  Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, Sadio Mane na mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Merick Aubameyang ndio wachezaji watatu wa mwisho wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika. Orodha hiyo ni marudio ya wachezaji watatu waliotajwa kuwania tuzo ya msimu uliopita, ambapo itatolewa kwa kuzingatia kiwango cha mchezaji husika katika mwaka 2018. Pierre-Merick Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon, amefanikiwa kuwepo katika orodha hiyo kwa mara ya tano mfululizo sasa, tangu mwaka 2014 na kuifikia rekodi ya mkongwe wa Ivory Coast, Yaya Toure na wa Ghana, Michael Essien. Mohamed Salah ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Misri kushinda tuzo hiyo tangu ilipoasisiwa mwaka 1992 na kutajwa katika orodha ya wachezaji watatu wa mwisho kwa miaka miwili mfululizo huku akishinda kwa mara ya kwanza msimu uliopita. Kwa upande wa Sadio Mane, ametajwa katika orodha hiyo kwa mwaka wa tatu mfululizo huku akiwa hajashinda tuzo hiyo mpaka sasa. Kilele cha tuzo hizo kinatarajiwa kufanyika Januari 8, 2019 mjini Dakar, Senegal.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako