• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Masumbwi: Mayweather atengua ahadi yake ya kutwangana tena na Manny Pacquiao

  (GMT+08:00) 2019-01-02 09:04:56

  Bondia, Floyd Mayweather, ametengua ahadi yake ya awali kwa Mfilipino, Manny Pacquiao na kuzima ndoto ya bondia huyo ya kukutana naye tena ulingoni. Mayweather ambaye mwezi Novemba alikutana na Pacquiao nchini Japan na kukubaliana watapigana tena, ametengua ahadi hiyo baada ya kumpiga Mjapani, Tenshin Nasukawa. Kauli hiyo imemuacha Pacquiao ambaye anatarajia kupigana na Andrien Broner, Januari 19 akitegemea kuwa baada ya kushinda pambano hilo atakutana ulingoni na Mayweather kwa pambano la marudiano kama walivyokubaliana. Mayweather alimpiga Pacquiao Mei 2015, lakini, Pacquiao alidai alipigana akiwa na majeraha ya bega aliyoyapata wakati wa mazoezi. Alifanyiwa upasuaji siku chache baada ya pambano hilo, hivyo alitaka lifanyike pambano jengine kati yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako