• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Juventus wapo vizuri zaidi kumnasa Aaron Ramsey baada ya kumaliza mkataba wake na Arsenal

  (GMT+08:00) 2019-01-02 09:05:49

  Juventus wapo vizuri zaidi kumnasa Aaron Ramsey baada ya kumaliza mkataba wake na Arsenal. Mabingwa hao wa Italia wanajiamini kumkamata mchezaji huyo wa kimataifa wa Weles juu ya dili la pauni 140,000 kwa wiki pamoja na pauni milioni 12 za kusaini. Bayern Munich na PSG pia zinafahamika kuvutiwa na kiungo huyo. PSG pia inampigia hesabu beki wa Tottenham Hotspurs, Toby Alderweireld ambapo anakipigia hesabu kifungu cha pauni milioni 25 cha kutolewa kwake. Jitihada yoyote ya ofa italazimika kusubiri hadi mwisho wa msimu. Naye kiungo wa kati wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil, 30, amesema hataihama klabu yake ya Arsenal kwa mkopo mwezi huu wa Januari. Badala yake, amesema yuko tayari kusalia kupigania nafasi yake katika kikosi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako