Huu ni mwaka wa Maadhimisho ya miaka 40 tangu Bunge la umma la China litangaze "Taarifa kwa Ndugu wa Taiwan". Sherehe kubwa zimefanyika leo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing, kuadhimisha kutolewa kwa taarifa hiyo. Rais Xi Jinping akihutubia sherehe hiyo amesisitiza kuwa muungano wa taifa la China ni mahitaji ya lazima ya ustawi wa taifa.
Kwenye sherehe iliyofanyika leo rais Xi ameeleza kuwa, tangu mwaka 1949, Chama cha Kikomunisti cha China pamoja na serikali na watu wa China siku zote zinachukua ufumbuzi wa suala la Taiwan, kutimiza muungano wa taifa kuwa jukumu lao la kihistoria, siku zote zinapunguza hali ya wasiwasi ya kando mbili za mlango bahari wa Taiwan, na kuelekea kwenye njia ya kujiendeleza kwa amani, ili kuzidi kupata maendeleo mapya. Rais Xi anasema:
"Historia na ukweli wa mambo kwamba Taiwan ni sehemu ya ardhi ya China, kando mbili za mlango bahari wa Taiwan ni ardhi ya China ambayo haiwezi kutwaliwa na mtu au nguvu yoyote; ukweli kwamba wakazi wa pande hizo mbili wote ni wachina, hisia ya asili kati ya pande hizo mbili hazitabadiliswa na mtu au nguvu yoyote! Mkondo wa mlango bahari wa Taiwan kuelekea kwenye hali yenye utulivu na amani, huku uhusiano kati ya pande hizo mbili ukipata maendeleo mapya hautabadilishwa na mtu au nguvu yoyote! Mwendelezo wa ustawi wa nchi, kuimarika kwa taifa na muungano wa kando mbili za mlango bahari wa Taiwan hazitabadilishwa na mtu au nguvu yoyote!"
Rais Xi ameeleza kuwa, ni lazima China ipate muungano na hakika itatimiza muungano. Huo ni mwelekeo wa kihistoria kwa kufuata mchakato wa maendeleo ya uhusiano kati ya kando mbili za mlango bahari wa Taiwan katika miaka 70 iliyopita, pia ni mahitaji ya lazima kwa ustawi wa taifa la China katika zama mpya. Katika mchakato wa taifa la China kupata ustawi, wakazi wa kando mbili za mlango bahari wa Taiwan wanapaswa kubeba majukumu ya kupata ustawi wa taifa, na kunufaika na fahari ya ustawi wa taifa. Amesisitiza kuwa mfumo tofauti si kikwazo kwa muungano wa taifa, wala si kisingizio cha kuleta mfarakano. Inatakiwa kutafuta mpango wa "Nchi moja, Mifumo Miwili" kuhusu suala la Taiwan. Anasema:
"Lengo la mpango wa 'Nchi Moja Mifumo Miwili' ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya wakazi wa Taiwan kulingana na hali halisi ya Taiwan. Utekelezaji halisi wa mpango huo utazingatia vya kutosha hali halisi ya Taiwan, kukusanya maoni na mapendekezo kutoka kando mbili za mlango bahari wa Taiwan, na kuzingatia vya kutosha maslahi ya wakazi wa Taiwan."
Rais Xi pia amesisitiza kuwa kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja ni kanuni ya kimsingi ya kimataifa ambayo inakubaliwa na jumuiya ya kimataifa. Kutimiza muungano wa taifa la China hakutaharibu maslahi halali ya nchi yoyote ikiwemo Taiwan, bali kutaleta fursa nyingi zaidi kimaendeleo kwa nchi mbalimbali duniani, na kuchangia katika kulinda utulivu na ustawi wa kanda ya Aisa na Pasifiki na dunia nzima, kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, pamoja na maendeleo ya amani ya dunia na maendeleo ya binadamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |