• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AfDB kuchangisha zaidi ya $7B kutoka masoko ya mitaji kwa ajili ya uwekezaji katika chumi za Afrika

  (GMT+08:00) 2019-01-02 19:46:33

  Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika imepitisha mpango wa mikopo wa taasisi hiyo wa mwaka 2019 wa US$7.24 bilioni kutoka masoko ya mitaji.

  Benki hiyo inapata masoko mingi ya mitaji na mikopo mingi wanayotoa ikiwa katika sarafu za dola za marekani na euro pamoja na utoaji katika masoko mengine ya umma kama vile dola za asutralia na Pound Streling.

  Taasisi hiyo kuu ya ufadhili wa maendeleo barani Afrika inasema kuwa ina wigo mkubwa katika jukwaa la uwekezaji na inaendelea kuwa mtoaji wa kawaida wa dhamana.

  Bidhaa hizi zinakidhi mahitaji ya uwekezaji na pia kuruhusu Benki hiyo kuonyesha mamlaka yake ya maendeleo na kukuza ukuaji endelevu na jumuishi.

  Mweka Hazina wa Benki hiyo,Hassatou N'Sele amesema benki hiyo itaendelea kukuza maendeleo ya masoko ya mitaji Afrika kwa kutoa madeni ya sarafu za ndani ili kufanikisha ufadhili wa shughuli za sarafu za ndani,pamoja na mipango mingine.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako