• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taiwan haitakosekana katika mchakato wa ustawishaji wa taifa la China

    (GMT+08:00) 2019-01-02 19:55:15

    Rais Xi Jinping leo ametoa hotuba muhimu katika sherehe ya kuadhimisha miaka 40 tangu serikali ya China itangaze "Taarifa kwa Ndugu wa Taiwan", huku akikumbusha historia ya maendeleo ya uhusiano kati ya kando mbili za mlango bahari wa Taiwan katika miaka 70 iliyopita. Ametoa mapendekezo matano kuhusu kuhimiza maendeleo ya amani ya uhusiano huo katika zama mpya, kuhimiza muungano wa amani wa taifa, huku akisisitiza kuwa ni lazima China ipate muungano na hakika itatimiza muungano, Taiwan haitakosekana katika mchakato wa ustawishaji wa taifa la China na muungano wa China utaleta fursa nyingi zaidi za maendeleo kwa nchi mbalimbali duniani.

    Hotuba hiyo imeonesha udhati na wema mkubwa wa kufanya juhudi kutimiza umoja wa amani wa China, ambayo pia imetoa onyo kali kwa wanaojaribu kuitenganisha Taiwan kutoka China na nguvu ya nje inayotaka kuingilia kati mambo ya Taiwan. Vilevile hotuba hiyo pia imeonesha nia thabiti ya chama tawala cha China CPC na serikali ya China kulinda mamlaka na ukamilifu wa ardhi, na kutoa mwongozo wa msingi kwa China kutimiza umoja wa taifa katika zama mpya.

    Katika miaka 40 iliyopita, kamati ya kudumu ya bunge la umma la China ilipotoa "Ujumbe kwa Ndugu wa Taiwan", haki zote halali za Jamhuri ya watu wa China zimerejeshwa katika hali ya kawaida kwenye Umoja wa Mataifa, na jumuiya ya kimataifa imetambua Taiwan ni sehemu isiyotengeka na China. Katika hali ya wakati ule, "Ujumbe kwa Ndugu wa Taiwan" imesisitiza kushikilia msimamo wa kuwepo kwa China Moja, huku ikipendekeza kumaliza hali ya mvutano wa kijeshi kati ya kando mbili za mlango bahari wa Taiwan, kufungua mawasiliano ya posta, biashara na usafiri, kupanua mawasiliano kati ya pande mbili katika sekta mbalimbali ili kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kuingia katika kipindi cha maendeleo ya umoja wa amani.

    Kupitia utekelezaji wa miaka 40 wa mageuzi na ufunguaji mlango wazi, China imeingia katika zama mpya, ambayo inakaribia zaidi kutimiza ustawi wa taifa la China kuliko wakati wowote, pia imekuwa na sharti na msingi wa kuhimiza mchakato wa umoja wa amani. Vyombo vya habari vya Taiwan pia China bara imeshika imara uongozi na udhibiti wa maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili.

    Hivi sasa, wachina wanafanya juhudi kutimiza ndoto na watu wa Taiwan wakiwa sehemu ya wachina pia hawawezi kukosekana na hawatakosekana katika mchakato huo. Kama rais Xi alivyosema, siku za mbele za Taiwan zinategemea umoja wa taifa, na ustawi wa Taiwan unatokana na ustawi wa taifa la China. Suala la Taiwan litatatuliwa kufuatia ustawi wa taifa!

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako