• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Chelsea yakamilisha usajili wa Christian Pulisic

  (GMT+08:00) 2019-01-03 09:19:27

  Klabu ya Chelsea jana ilitangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Marekani na klabu ya Borussia Dortmund Christian Pulisic kwa dau linalotajwa kufikia pound milioni 58. Pulisic ambaye alikuwa anawaniwa na Liverpool atajiunga na Chelsea mwisho wa msimu. Christian Pulisic mwenye umri wa miaka 20 amekuwa ni miongoni mwa viungo mahiri wa Dortmund toka ajiunge na klabu hiyo mwaka 2015 akitokea PA Classic lakini akiichezea Dortmund mechi 115 na kupachika magoli 15, timu ya taifa ya Marekani akicheza michezo 20 na kufunga magoli 9. Kiungo huyo atamalizia msimu akiwa na Borussia Dortmund wakati ambao Eden Hazard akiwa kabakiza miezi 12 katika mkataba wake na Chelsea, kwani bado anachelewa kufanya maamuzi kama ya aendelee kusalia Stamford Bridge au aondoke ila inaripotiwa kuwa atakuwa anasubiria ofa kutoka Real Madrid.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako