Waziri wa mambo ya ndani ya Sudan Bw. Musa Ali Madibo amesema hali ya usalama ya nchi bado ni nzuri.
Bw. Madibo amesema sheria za Sudan zimehakikisha haki ya watu kufanya maandamano chini ya ruhusa kutoka serikalini, na kutoiletea nchi uasi na ghasia ambazo zitaathiri utulivu wa nchini. Pia amewahimiza watu kusaidia kuzuia wale wanaolenga kuhujumu usalama na utulivu wa nchi.
Habari zinasema, bunge la Sudan limepitisha amri za rais kurefusha hali ya dharura katika majimbo ya Kassala na Kordofan Kaskazini hadi tarehe 20 Juni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |